Jumatano 4 Juni 2025 - 17:24
Imam Khomeini alikuwa ni mchanganyiko kamili wa elimu na matendo

Hawza/ Ayatollah Jawadi Amoli amesema: Imamu Khomeini (ra) alielewa kwa usahihi kila alichokifahamu, na alitenda kwa usahihi kila alichokitenda. Alikuwa ni mtu aliyekusanya kwa ukamilifu kati ya elimu na matendo; hivyo basi, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, hakukuonekana na dosari yoyote katika mipango ya kielimu wala katika mipango ya kimatendo ya mtu huyu mkubwa wa kimungu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Jawadi Amoli, katika andiko aliloandika kuhusiana na kumbukumbu ya mwaka wa kufariki kwa Imamu Khomeini, amesema:

“Imamu wa Umma (ra) aliunganisha kwa usahihi baina ya elimu ya kiakili (maʿqul) na elimu ya mapokezi (manqul), na baina ya elimu ya mashuhuda (mashhud). Alikusanya kwa usahihi kati ya elimu na matendo, kati ya fikra na msukumo wa kiroho. Alielewa kwa usahihi kila alichokifahamu, na alitenda kwa usahihi kila alichokitenda. Hapakuwa na kutengana kati ya elimu yake na matendo yake, wala matendo yake na elimu yake. Alikuwa ni mchanganyiko kamili wa elimu na matendo kwa njia sahihi; alikusanya kwa usahihi kati ya akili, mapokezi na mashuhuda; alikusanya kwa usahihi kati ya siasa, busara, usimamizi na ufakihi. Hivyo basi, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, hakukuonekana dosari yeyote katika mipango ya kielimu wala katika mipango ya kimatendo ya mtu huyu mkubwa wa kimungu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha